MVUA KUBWA YA UPEPO YASABABISHA MAAFA MKOANI SHINYANGA
Mvua kubwa ya upepo mkali
imesababisha maafa katika vijiji vya Ukenyenge na Negezi wilayani
Kishapu mkoani Shinyanga ambapo imeezua paa za nyumba 37 pamoja na
majengo Serikali.
Tukio hilo lilitokea saa 12 jioni
ambapo majengo yaliyopatwa na maafa hayo ni ya pamoja na ofisi ya tarafa
ya Negezi, ofisi ya afisa kilimo, ofisi ya TCRS.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu,
Sahadrack Kengese alitembelea eneo hilo yalipotokea maafa akiwa
amembatana na wataalamu kutoka halmashauri kwa ajili ya kufanya
tathimini ya tukio hilo.
Mratibu wa Maafa Wilaya, Ponsian
Kuhabwa na Mwesiga Katunzi kutoka Idara ya Ujenzi waliungana na viongozi
wa tarafa na kata na kufanya tathimini hiyo ambapo bado hasara
iliyotokea haijafahamika.
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa
Tarafa, David Isanga mara baada ya tukio hilo uongozi wa tarafa na kata
ulishirikiana na wananchi kuhakikisha wanawasaidia wenzao walioathirika
ili kurudisha hali.
Tathimini inaonesha kuwa hali ya
maafa sio ya kutisha na ipo katika uwezo wa jamii kusaidiana na kuwa
katika jengo la tarafa inaonyesha mahitaji mbalimbali ili kulirudisha
katika matumizi.
Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ni
pamoja na ukarabati kufanyika haraka ili watumishi wapate sehemu za
kufanyia kazi kwani sasa hivi wanabanana katika vyumba viwili
vilivyosalimika.
Aidha, timu ya tathmini ilishauri
kuendelea kupanda miti mbele ya jengo hilo ili kupunguza kasi ya upepo
na kutunza mazingira katika eneo hilo. Pia wananchi wameshauriwa kupanda
miti na kujenga nyumba imara ambazo zitasitahimili mitikisiko ya
matukio kama haya.
No comments