Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo Disemba 2017,
amemkabidhi Rais John Pombe Magufuli takwimu inayoonyesha hali ya
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), wakati wa uwekaji wa jiwe la
msingi katika ofisi za Takwimu Mjini Dodoma.
Dkt. Mpango amesema kuwa takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya
Takwimu ya Taifa juu ya hali ya maambukizi ya VVU, inaonyesha kuwa Mkoa
wa Njombe ndo unaoongoza kwa maambukizi ya VVU, na utafiti huo
uliwahusisha watu wenye umri wa miaka 15-49 kwa mwaka 2016-17.
"Kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za
Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na Njombe 11.6%, Iringa 11.2% na
Mbeya 9.2%. Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni Unguja 0%,
Kaskazini Pemba 0%, Lindi 0.3%, Manyara 1.8% na Arusha 1.9%.", amesema
Dkt. Mpango.
Mara baada ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo Rais Magufuli amewataka
wananchi kupuuzia watu wanaotoa takwimu za uongo, na kusema kwamba wenye
mamlaka ya kutoa takwimu za taifa ni ofisi ya Taifa ya Takwimu pekee.
No comments