BASI la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake
kati ya Kaisho, Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la
Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha kifo cha kondakta
wa basi hilo.
Kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo
hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali teule ya
Nyakahanga na wengine katika Kituo cha Afya Nkwenda kilicho karibu na
eneo la ajali.
No comments