Mtu mmoja wilayani Mkalama Singida aliyefahamika kwa majina ya Mpanda
Jumapili (35) auawa kwa kuchomwa kisu kifuani na Daudi Labani kwa ugomvi
wa shilingi 4000 uliotokea kwenye michezo ya kubahatisha.
Akiongea na www.eatv.tv Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa chanzo cha kifo hicho ulikuwa ni ugomvi
ulioanzia kwenye ugomvi mchezo wa kubahatisha.
"Mtuhumiwa pamoja na marehemu walikuwa wanacheza mchezo wa kubahatisha
katika mashine ya kichina kwa hiyo mzozo ulianzia maeneo hayo wakatoana
nje na mtuhumiwa aliweza kumchoma kisu marehemu upande wa kushoto
kufuani, alikimbizwa hospitali na mauti ulimkuta akiwa hospitali hivyo
baada ya wananchi ambao walikuwa pale walipoona hilo tukio walimkamata
huyo mtuhumiwa na kutoa taarifa kituo cha polisi lakini wakiwa
wanaelekea kituoni lilijitokeza kundi jingine kwa nyuma likiwarushia
mawe na fimbo na walipokaribia kituoni jiwe moja lilimpata huyo
mtuhumiwa kichwani akaanguka hapo hapo"
Kamanda aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa
"Baada ya yule mtuhumiwa kuanguka wale wananchi waliendelea kurusha mawe
na kuharibu baadhi ya vitu katika kituo cha polisi na kuharibu taa nne
na kuvunja madirisha mawili ya vioo ya kituo cha polisi, huyo mtuhumiwa
mpaka sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu kufuatia majeraha
aliyopata kwa kipigo cha wananchi" alisema Deborah
No comments