Father Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohana Mbatizaji Ruhanga ambaye
ameendesha ibada ya kuaga mwili wa marehemu Akwilina katika Chuo cha
Usafirishaji (NIT) amemtaka aliyetekeleza mauaji ya mwanafunzi huyo
aliombe msamaha Taifa.
Father Raymond amesema hayo leo Februari 22, 2018 na kudai kuwa jukumu
hilo wameiachia serikali ya awamu ya tano na vyombo vyake vya usalama
kuwa endapo watampata mtu huyo wahakikishe kuwa analiomba taifa msamaha
kwani kitendo alichofanya kimewaumiza Watanzania hivyo hata akifungwa
miaka 30 haitasaidia kwa kuwa tayari Akwilina ametangulia mbele ya haki
na hatoweza kurudi.
"Mimi kama mtoto wa Mungu kama wengine walivyo watoto wa Mungu niwaombe
tufanye kazi ya upatanishi na naomba wale ambao wana hiyo nafasi na kwa
hili lililotokea kwa mwanetu Akwilina limetuumiza na kwa jinsi
lilivyotuumiza nafikiri linahitaji kuponywa na namna moja tu ya
kuliponya tunawaomba wale wahusika ambao wana madaraka ya kuweza
kulisaidia. Huyu aliyefanya kitendo hiki baada ya kujulikana aliombe
taifa hili msamaha ni hicho tu hatuna namna nyingine hata tukimfunga
miaka 30 au 40 Akwilina hawezi kurudi amekwenda lakini aliyefanya huenda
kwa nia nzuri ikitakoea bahati mbaya tunaomba vyombo vinavyohusika
vikimaliza utaratibu wake akajulikana huyo mtu hata kwa kupitia TV
awaombe wana Mungu msamaha" alisema Father Raymond
Father Raymond aliendelea kusema kuwa
"Kheri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu vinginevyo
hatutafika mbali, tumuombe Mungu kila mmoja wetu katika imani yake leo
ni Akwilina huenda kesho itakuwa ni wewe sasa hatutaki hilo liendelee,
na hilo halitaendelea tu kama mtu atakubali kuomba msamaha
kujinyenyekeza, kuwa mnyenyekevu na kukubali nimekosa mimi, nimekosa
sana nawaomba msamaha kwisha tunaendelea kama familia hakuna asiyekosea.
Lakini unapojaribu kutafuta mbinu ukaliweka hivi unaliweka vile unazidi
kuumiza kwa sababu mimi kama mzazi sitaelewa
"Naomba nisema hapa bila hata kigugumizi nafikiri wenye nafasi hii si
wengine ni serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaiomba
kama ilivyojitolea kuweka haya mazishi katika level hiyo, tunawaomba pia
watusaidie kwa sababu wao ndiyo wamepewa dhamana ya maisha yetu wote
hapa, na sisi kama watoto wa familia hatulingani kama vidole vyetu
tunaimani kwamba serikali yetu itatusaidia katika kulipatanisha, katika
kurudi kufanya kazi kama watoto wa familia moja"
No comments