Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limewapanga waamuzi kutoka
nchini Afrika Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho barani
Afrika wakati Simba itakapocheza na Al Masry ya Misri Machi 7, 2018
uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele
Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi
msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher
Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka
Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea.
Mwamuzi wa kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom
Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase
mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane
Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo atatoka Libya Gamal Salem
Embaia.
No comments