Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO akutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo
Na Koleta Njelekela, STAMICO
Kaimu
Mkurugenzi wa STAMICO Mhandisi John Nayopa amekutana na Mkurugenzi wa
Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.
Hassan Abbas, ambaye alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya STAMICO
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana naye na kuzungumzia namna
ya kuimarisha ushirikianao katika upashanaji habari za STAMICO kwa
Watanzania.
Viongozi
hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika suala zima la
kuelimisha Watanzania kuhusu shughuli za STAMICO kwa kutumia mitandao ya
kijaamii (Social Media) ya Idara ya Habari Maelezo, Jarida la Nchi
yetu linaloratibiwa na Idara hiyo na Vyombo vya Habari kwa ujumla.
Aidha
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dakta Abbasi amesema Idara yake
iko tayari kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kwa
Umma wa STAMICO katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji yao, ili
kuwajengea uwezo zaidi katika taaluma zao.
“
Kulingana na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Idara yangu
inaweza kutoa mafunzo ya kuanzia kwa wataalamu wako kuhusu Sayansi ya
Mitandao ya Kijamii na uendeshaji wake; Mawasiliano kwa Umma wakati wa
Majanga (Crisis Communication); pamoja na Sera na Miongozo ya matumizi
ya Mitandao ya Kijamii” Alifafanua Dk. Abbasi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Nayopa amemshukuru Dakta.
Abbasi kwa kumtembelea ofisini kwake na ameahidi kuimarisha ushirikiano
na Idara ya Habari Maelezo katika kuelimisha Watanzania kuhusu mchango
wa STAMICO katika kuleta matokeo chanya kwenye Serikali ya awamu ya
tano.
Kaimu
Mkurugenzi wa STAMICO, Mhandisi John Nayopa akipata maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Hassan Abbas, kuhusu majukumu ya Idara ya Habari Maelezo na Mfumo wa
Upashanaji Habari na Mawasiliano Serikalini ofisini kwake jijini Dar es
Salaam .
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan
Abbasi (kushoto) akikabidhi Jarida la Nchi Yetu toleo la Novemba 2017
kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa
alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Jarida
hilo linaratibiwa na Idara ya Habari Maelezo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakta Hassan
Abbasi (kushoto) akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu Jarida la Nchi Yetu
toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi
John Nayopa alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi
karibuni.



No comments