Linah ataja idadi ya wanaume aliyowahi ku-date nao tangu awe maarufu
Msanii wa Bongo Fleva, Linah ameamua kuweka wazi kwa kutaja idadi ya wanaume ambao alishawahi kudate nao tangu awe maarufu huku akishindwa kukumbuka wanaume ambao alikuwa nao kipindi hicho kabla ya kupata jina.
Linah
“Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume watano hivi toka hivi watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa,“amesema Linah kwenye mahojiano yake na EATV kwenye kipindi cha Kikaangoni.
Hata hivyo, Linah amesema idadi hiyo ya wanaume ni baada ya kupata jina ila wale aliyowahi kutoka nao kimapenzi kipindi cha nyuma kabla ya umaarufu hawakumbuki ila ni kati ya 10 au 15.
No comments