Makonda apokea Makontena 20 ya vifaa vya Walimu Dar
RC Makonda amesema kuwa jumla ya Makontena 36 yanatarajiwa kuwasili ambapo leo yamepokelewa 20 na makontena 16 yanatarajiwa kuwasili bandarini ili kusambaza katika ofisi mpya 402 ambazo zinajengwa.
Amesema hayo katika uzinduzi uliofanyika kurasini, Temeke jijini Da es salaam na kuwa Serikali ilijisahau kuwajengea walimu ofisi badala yake walishughulika na ujenzi wa Madarasa na vyoo vya shule pekee na kuwa sahau walimu ambao ndiyo mhimili mkuu na muhimu katika jamii.
"wakati mwingine matatizo ambayo yanatusumbua yame sababishwa na sisi wakuu wa idara tumezembea mahalani mimi nashukuru Sana kutafuta kwa aliyekuwa Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Mhe kwa kuwa alikuwa hashughuliki na changamoto za walimu" amesema
Aidha ametaka walimu kuthaminiwa kama ilivyokuwa zamani na hivyo atatoa waraka rasmi ili walimu wapewe kipaumbele katika huduma za kijamaa na wasipange foleni, huku akiwa omba walimu kufundisha wanafunzi kwa moyo ili yaweze kupatikana matokeo mazuri kama mwaka jana.
Pia amewashukuru wote walio jitolea ili kufanikisha usafirishaji wa Makontena hayo wakiwemo Bank ya walimu (MCB) na Mfanyabiashara wa Makontena Emanuel Malya kwa kujitolea eneo lake na kulipia usafiri wa Makontena matatu.
Hata hivyo ameendelea kuwashukuru watu wa Marekani walijitoa samani hizo na kuwaombea kwa mwenyezi Mungu awazidishie, pamoja na waandishi wa habari kwa kuandika habari zilizowafanya wafadhili sehemu mbalimbali ulimwenguni kufahamu mahitaji ya walimu.




No comments