Mbunge asekwa rumande saa 48 kwa amri ya mkuu wa wilaya
Mbunge wa Tunduma, wilayani Momba mkoani
Songwe, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi kisha kuwekwa mahabasu kwa
saa 48 kwa kile kinachodaiwa ni amri ya mkuu wa wilaya hiyo, Jumaa
Irando.
Akizungumza na gazeti hili leo Februari
21, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe,
Ayub Sikagonamo amesema Mwakajoka amekamatwa akiwa kituo cha polisi
Tunduma kuitikia wito wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD) baada ya
kumpigia simu kwamba anamhitaji ofisini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange alisema ‘Nipo nje ya ofisi, in-short’ kisha akakata simu.
Hii ni mara ya pili kwa Mbunge Mwakajoka
kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 48 kwa amri ya mkuu huyo wa
wilaya. Agosti mwaka jana Irando aliamuru kukamatwa Mwakajoka kwa kile
alichodai alitoa lugha ya kumdhalilisha yeye na Serikali ya Mkoa wa
Songwe wakati akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Na Godfrey Kahango, Mwananchi

No comments