Mwigulu Nchemba Awakemea Wanasiasa Wanaoihusisha Serikali na Kushambuliwa kwa Tundu Lissu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka
wanasiasa kuacha kutumia kuumia kwa mbunge Tundu Lissu kama chambo ya
kisiasa katika majukwaa.
Dkt. Mwigulu amesema hayo jana mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mitunduluni.
Mwigulu amewataka wanasiasa waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama
mitaji ya kisiasa badala yake waje na hoja za maana za kusaidia katika
maendeleo ya nchi.
Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo
kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa ambao hawakuwa
hata na shida na mtu yoyote na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa je
serikali ndio imehusika.
“Sisi tunaoshughulika na maswala ya uhalifu tunatafuta wahalifu
wanaofanya maswala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni ajenda ya kisiasa
wakati sisi tunaombea mtu apone” alisema Dkt. Mwigulu
Dkt. Mwigulu ameongeza na kusema kuwa je angeamua kuendelea kusema
kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki inauhusiano gani na shida za
kata ya Mitundulini, hivyo wananchi wa Singida wawaadhibu kwa kuwanyima
kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.
Uchaguzi mdogo katika kata ya Mitunduluni unafanyika baada ya Diwani aleyekuwepo katika kata hiyo kufariki dunia kwa maradhi.
VIDEO:

No comments