Utajuaje Kama Girlfriend Wako Anakupenda ? Dalili Na Ishara Zote Tunazo Hapa
Unaweza
kuwa na girlfriend kwa muda mrefu na usiweze kujua kama anakupenda au
la. Wanawake wengine wanaweza kujifanya girlfriend wazuri kumbe
wanakutumia. Na pia unaweza kuwa na girlfriend halisi ambaye anakupenda
kuanzia juu mpaka chini.
Kama mwanaume, unapaswa kujua ishara zote ambazo zinaonyesha iwapo mwanamke anakupenda ama anakutenda. Hii ni muhimu kwa kuwa utakuwa unasoma vigezo vyake ili uweke uamuzi wa mwisho kama iwapo utakubali kuishi na yeye milele ama utaamua kumuacha katikati.
Hapa Nesi Mapenzi leo tumekuletea ishara zote ambazo zitakuonyesha iwapo mwanamke/girlfriend wako anakupenda au la. Zama nasi.
Kama mwanaume, unapaswa kujua ishara zote ambazo zinaonyesha iwapo mwanamke anakupenda ama anakutenda. Hii ni muhimu kwa kuwa utakuwa unasoma vigezo vyake ili uweke uamuzi wa mwisho kama iwapo utakubali kuishi na yeye milele ama utaamua kumuacha katikati.
Hapa Nesi Mapenzi leo tumekuletea ishara zote ambazo zitakuonyesha iwapo mwanamke/girlfriend wako anakupenda au la. Zama nasi.
Ishara kuonyesha kama mwanamke/girlfriend wako anakupenda.
#1 Anakufanyia yale mambo madogo madogo kuyafanya maisha yako kuwa rahisi. Kama
mwanamke anakupenda basi jambo la kwanza la kufanya ni kuonyesha upendo
kwa anayempenda. Kama unamwona anakukunjia nguo zako, anakutembelea
kuhakikisha nyumba yako iko safi ama kuhakikisha hausahau kununua kitu
muhimu kwa nyumba yako basi ujue anakupenda.
#2 Anakuoshea nguo. Kama
anakufanyia kitu nyumbani kwako ambacho yeye mwenyewe huwa hapendi
kufanya kwake basi ni ishara nzuri. Anajaribu kuonyesha uanawake wake
kinyumba. Katika DNA ya mwanamke ni kuwa ameumbwa kuwajali wale ambao
anawapenda ili kuwarahisia maisha. Kama girlfriend wako anaonyesha hizi
tabia basi ujue anakupenda.
#3 Kando na kuwa anajua chakula unachokipenda, anajaribu kukitengeneza. Anajua chakula nachokipenda? Ashawahi kukutengezea mara kwa mara? Huyo anakuonyesha kuwa anakupenda.
#4 Anaelewana na familia na marafiki zako hata kama hawamthamini. Kama
girlfriend wako anatabasamu hata kama familia yako inachukiza, basi huo
ni upendo. Kwa kawaida wanawake hawaelewani na familia ya mwanaume.
Lakini ukiona anajaribu bila kulalamika, hio ni ishara ya upendo kwako.
#5 Anakatiza shughli zake kuja kukuona. Kama
yuko tayari kuuza tiketi yake ya kwenda kwa concert ya Diamond ili
aspend usiku na wewe, hio ni ishara ya kukuambia, "nakupenda."
#6 Anayaweka matakwa yako mbele. Ukiona
yuko tayari kufunja sherehe na marafiki zake ili asherehekee na familia
yako ama kwenda kula dinner na marafiki zako ni ishara ya mapenzi.
#7 Anakusifia pale ambapo inahitajika. Mwanamke
ambaye anakupenda hataona tatizo kukusifia pale ambapo kunahitajika.
Kuambia mtu kuwa unampenda kunaonyesha kuwa unamthamini.
#8 Ni mtu wa kwanza kukupigia iwapo ana furaha, huzuni ama hasira. Kitu
chochote ambacho kitamtokea yeye atakuwa wa kwanza kukuambia. Hii
inamaanisha anakupenda na anakuamini. Uwepo wako kwake anaudhamini na
kuuzingatia.
#9 Atakwambia mambo ambayo hayapenda. Ashawahi
kukuambia mambo yaliyomuaibisha, huzunisha ama kumfelisha? Ukiona
anakwambia kila kitu hata siri zake za kuzimu basi fahamu kuwa
anakupenda.
#10 Anaonyesha ukichaa wake. Hakuna
mtu anaweza kufunguka asilimia 100 tabia zake kwa yeyote. Ukiona
amekuwa huru na wewe kiasi cha kuwa anaweza kuachilia hewa, kukuonyesha
sura za kiajabu, ama kufanya mambo ambayo hukutarajia, basi ni ishara ya
kuwa penzi lake kwako ni la dhati.
#11 Anashikwa na wivu ukiongea kuhusu wanawake wengine, lakini si sana. Mwanamke anayekupenda huwa hapendi kuskia ukiwasifu wanawake wengine. Hio ni kawaida.
Hizi
ni baadhi ya dalili kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda. Je girlfriend
wako anaonyesha hizi tabia ama ni mtofauti na tabia hizi tulizozitaja?
Uamuzi ni wako sasa.

No comments