Header Ads

Fahamu: Idadi ya ngoma zilizopo kwenye albamu ya ‘LADHA’ ya Chin Bees



Msanii wa muziki bongo miondoko ya Trap, Chin Bees ameweka bayana ngoma zitakazopatikana katika albamu yake ya ‘Ladha’ inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Ijumaa ya wiki hii (Kesho).

Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Bees ameweka orodha kamili ya ngoma hizo 11 zitakazokuwepo humo.

Kwenye uzinduzi huo ambao utafanyika Club Next Door jijini Dar es Salaam, utahudhuriwa na mastaa kibao, Bees pia atagawa bure nakala za album hiyo kwa mashabiki watakaohudhuria pamoja na kuionesha kwa mara ya kwanza video ya wimbo wake mpya.
Katika kipindi cha miaka miwili, Chin Bees anayetokea Arusha, ameibuka kuwa mmoja wa waimbaji waliochupikia kwa kasi huku nyimbo zake Pepeta, Kababaye, Nyonga na zingine zikimweka juu.

No comments

Powered by Blogger.