Header Ads

Kesi ya Nabii Tito yaahirishwa



Kesi ya kujaribu kujiua inayomkabili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, imeahirishwa hadi  Machi 19, 2018.

Awali hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili yake ili kujua kama ana matatizo ya akili katika taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma.

Hata hivyo, Nabii Tito hakuweza kufika mahakamani leo Machi 5, 2018 ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Mwajuma Lukindo baada ya hakimu anayesikiliza kesi yake, James Karayemaha kutokuwepo mahakamani.

Nabii Tito alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari  29, 2018 na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wembe na anadaiwa kufanya hivyo Januari 25, 2018 akiwa mahabusu.

No comments

Powered by Blogger.