Msanii ambaye alifanya vizuri katika muziki kipindi cha nyuma kwa staili
yake ya Takeu, Mr Nice amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake kuimba
vitu vyenye msingi ili kusudi wasije kuwapotosha mashabiki zao
wanaowatazama.
Mr. Nice ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi
cha 'Bongo Flava Top 20' kinachorushwa na East Africa Radio baada ya
kupita siku chache kupita tokea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
kupeleka orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kwa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambazo zina maudhui ambayo ni kinyume na
maadili na Kanuni za Huduma ya Utangazaji ya mwaka 2005.
"Mimi ninachoweza kusema bila ya kuficha, vijana na watoto wadogo ndio
wanaopenda muziki sasa hivi, hivyo basi msanii atakapoimba kitu ambacho
hakina maana, adabu wala mantiki atakuwa anampotosha mtoto. Maana vijana
hao hao wanaosikiliza na kutazama muziki wetu wengine husema natamani
kuwa kama msanii fulani bila ya kujua mtu huyo anaimba matusi matupu
'so' unategemea nini hapo", amesema Mr. Nice.
No comments