Roma Mkatoliki apigwa ‘STOP’ kufanya muziki, Nay wa Mitego apewa onyo kali
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni imemfungia kifungo cha miezi sita msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki kutojihusisha na shughuli zozote za muziki baada ya kukaidi agizo la kubadilisha wimbo wake wa Kibamia.
Roma Mkatoliki
Mhe. Shonza amesema kuwa adhabu hiyo itajumuisha na nyimbo zake zote kutokupigwa Redioni wala kwenye runinga kwa muda wote aliyofungiwa.
Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema Serikali itaangalia mwenendo wa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ambaye naye aliitwa na kukiri makosa na kuahidi kubadilika.
No comments