SIMBA YADAMIRIA KUFANYA MAAJABU DHIDI YA AL MASRY, WAFANYA MAZOEZI YA AINA YAKE TU

Kikosi
cha Simba kimeonesha kweli kimedhamiria kuibuka na ushindi dhidi ya Al
Masry SC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho.
Katika
hali isiyo ya kawaida, kikosi hicho kilifanya mazoezi kuanzia majira ya
saa moja mpaka mbili usiku wa jana kwenye uwanja wa Boko Vetarani, Dar
es Salaam.
Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji wapo katika morali nzuri kuelekea mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 12 jioni.
Aidha wachezaji Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima wote walijumuika na wenzao kujifua kuelekea mechi hiyo kubwa.
Simba watafanya mazoezi ya mwisho leo kabla ya kuwavaa Al Masry jioni ya kesho
No comments