Tunahitaji mechi 5 kutwaa ubingwa EPL – Guardiola
Baada ya usiku wa jana siku ya Alhamisi meneja wa Manchester City, Pep Guardiola kutimiza mchezo wake wa 100 toka kuiyongoza timu hiyo na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 0 dhidi ya Arsenal, kocha huyo ametangaza dalili za kutwaa ubingwa wa EPL msimu huu.
Guardiola amesema kuwa wanahitaji michezo mitano tu ili kutwaa ubingwa wa ligi hiyo licha ya kuwa sijambo rahisi kuhakikisha wanalinda tofauti ya pointi 16 walizo nazo dhidi ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili.
Ni muhimu kuhakikisha tunazilinda pointi hizi 16 ambazo ni tofauti yetu na anayetufuatia, tunahitaji michezo mitano pekee ili tutangaze ubingwa .Msimamo wa ligi kuu ya Uingereza inaonyesha kuwa Man City inaongoza kwa kuwa na jumla ya alama 75 wakati nafasi ya pili ikishikiliwa na Man United yenye pointi 59.
Siyo rahisi, ukitwaa ubingwa usidhani unaweza kupumzika hapana ni lazima kuongeza juhudi maana tuna msimu waajabu katika ligi.
Tulipo cheza mara ya kwanza na Arsenal katika Carabao Cup hatukurudi nyuma lakini leo tumeweza kurudi nyuma na kuonyesha kiwango bora kabisa.
No comments