BREAKING NEWS: Zidane Ang'atuka Real Madrid
Siku tano baada ya Kocha Zinedine Zidane kuiongoza Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiifunga Liverpool magoli 3-1, hatimaye ameng'atuka katika nafasi hiyo,
Taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo zimesambaa kwa kasi huku kukiwa hakuna taarifa zozote zinazoonesha kwamba anaenda timu gani kwa ajili ya msimu ujao huku pia sababu za kujiuzulu zikiwa hazijulikani.
Zidane ametwaa mataji matatu mfululizo ya UEFA akiwa kama kocha mkuu na kueka rekodi ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo huku pia akitwaa taji hilo akiwa kama kocha msaidizi mwaka 2014 chini ya Carlo Ancellot na mwaka 2002 akitwaa kama mchezaji katika ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Chanzo: BBC

No comments