Header Ads

Mchungaji awaomba waumini wamchangie tsh bil. 123 anunue ndege binafsi


Mchungaji maarufu nchini Marekani, Jesse Duplantis amewaomba waumini wake kumchangia fedha kwa ajili ya kununua ndege yake binafsi ambayo itamsaida kueneza injili duniani kote kwa urahisi.

Jesse amesema kuwa anahitaji kiasi cha dola milioni $54 sawa na tsh bilioni 123.2 kununua ndege aina ya Falcoln 7X ambayo itamsaidia kutembea sehemu yoyote duniani.

Akiongea kupitia video iliyowekwa kwenye website rasmi ya kanisa lake la Christian Today amesema kuwa ameoteshwa na Mungu kuwa atapata aina hiyo ya ndege bila kutoa hata shilingi moja mfukoni mwake.

Kwenye video hiyo pia amemtolea mfano Bwana Yesu Kristo kuwa hata yeye angekuwa anaishi duniani hadi leo asingefanya kazi ya uinjilishaji kwa kusafiri na punda.

“Mpaka sasa naamini kuwa kuna watu hawataki kuona Wachungaji wakitumia ndege kueneza injili duniani, lakini hawatambui kuwa sauti pekee sio suluhu tunapaswa kuonana na waumini wetu kokote duniani. Kwani naamini hata Yesu angelikuwa duniani kwa sasa asingetumia usafiri wa Punda kwenda kueneza injili,“ameongea Mchungaji Jesse kwenye video hiyo.

Kupitia website yao (Christian Today) tayari watu wameanza kutoa michango yao. Hatua hiyo inakuja baada ya wiki mbili zilizopita Mchungaji mwingine aitwaye Kenneth Copeland kutoka Texas kuchangiwa kiasi cha dola milioni 36 kwa ajili ya kununua ndege.

Hata hivyo, Jesse anamiliki Jet nne na zote zimenunuliwa na Kanisa ila anataka aina nyingine ya  Falcoln 7X ambayo atakuwa na uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi bila kusimama njiani.



No comments

Powered by Blogger.