Vyama vya ushirika vyatakiwa kuajiri watendaji wenye elimu mzuri ili kuepuka hasara
Na Ahmad Mmow,Lindi
VYAMA vya Ushirika,hasa vya msingi (AMCOS) vimetakiwa kuajiri watendaji wenye elimu mzuri ili kuviepusha na hasara inayosababisha visiwe na maendeleo na kushindwa kuwahudumia wakulima ipasavyo.
Wito huo umetolewa na naibu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini, Charles Malunde alipozungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao uliofanyika jana katika manispaa ya Lindi.
Malunde alionya kuwa tabia yakubebana katika mambo yanayohitaji elimu na ujuzi katika utendaji hainabudi kuachwa.Badala yake uwezo na utendaji uwe msingi wakuteuliwa na kuchaguliwa mtu kuhudumu katika nafasi ya utendaji au uongozi.Badala ya kuwabeba watu wasio na uwezo kwasababu ya kufahamina,urafiki na udugu.
Alisema tabia ya kuteua na kuchagua watu wasio na uwezo kumesababisha matatizo na ugumu katika uendeshaji vyama na kusababisha hasara ambazo zinachangia vyama hivyo vishindwe kusonga mbele kimaendeleo.Badala yake vinasababisha malalamiko kutoka kwa wananchi kwenda kwa serikali.
Ofisa huyo wa juu wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini yenye mamlaka ya maendeleo ya vyama vya ushirika alisema sababu zinazotolewa ili kuhalalisha tabia ya insyofanywana baadhi ya vyama vya ushirika.Ikiwemo kukwepa gharama ya kuwalipa mishahara mikubwa haina maana.Kwasababu hasara inayosababishwa na watendaji wasio na elimu ya kutosha nikubwa kuliko fedha ambazo zingetumika kuwalipa mishahara wasomi.
"Sisemi nilazima wawe na elimu ya vyuo vikuu,lakini hivi sasa vijana wenye elimu ya vitado vya nne na sita wapo hadi vijijini.Niwengi,vyama vinashindwaje kuwaajiri,”alisema Malunde.
Alionya kwamba tabia ya vyama vya ushirika kusubiri serikali ipeleka miongozo ya kuvitaka vifanye mambo fulani ili viepuke hasara,wakati vyenyewe vinaona hasara haikubaliki.Huku akibainisha kwamba visisubiri kupelekewamwongozo wa kuvitaka viajiri watu wenye viwango vizuri vya elimu.
Alisema vyama hivyo kuwa na watendaji wasio na uwezo,licha ya vyenyewe kushindwa kupiga hatua ya maendeleo na kuchangia kujenga uchumi wa nchi.Lakini pia vinasababisha matatizo baina ya wakulima na serikali.Kwani wakulima wamekuwa wanailaumu serikali kutokana na matatizo yanayosababishwa na watendaji na viongozi wabovu.
Malunde licha ya kuvishukia vyama vya ushirika,aliwageukia wasomi nchini kwa kuwaasa wawe waadilifu pindi wapoaminiwa nakupewa nafasi ya kuwahudumia wananchi kutokana na elimu zao.Kwani ubora wa elimu yao unapimwa kutokana na ufanisi wakutekeleza majukumu yao kwa kuonesha tija katika jamii.
Alisema wasomi wanawajibu mkubwa wakuwa waadilifu wanapopewa nafasi ili jamii iweze kuwa na imani juu yao.Badala ya wao kuwa sehemu yawanaosababisha matatizo kwa jamii na nchi.Hasa ikizingatiwa elimu waliyonayo inatakiwa itumike na kuwanufaisha waTanzania wote.
Mbali na hayo,mkutano huo ulimchagua Mohamed Duka kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho kinachoundwa na vyama vya msingi(AMCOS) 39.Huku Rashid Masoud akichaguliwa kuhudumu kwa nafasi ya makamo mwenyekiti.

No comments