Header Ads

Waziri Majaliwa atoa pongezi kwa Mstahiki Meya kwa kuwapa mtaji Wajasiliamali



Serikali imewataka Wananchi wanaokaa pembezoni mwa mto msimbazi kuondoka kutokana na maendeleo ambayo yanatarajiwa kufanyika ikiwemo  kujengwa kwa ukuta ambao utazuia uharibifu wa mazingira. 

Hayo yamesemwa na waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa wiki ya utunzaji wa mazingira yenye kauli mbiu isemayo,  Mkaa ni gharama Tumia nishati mbadala.  Ambapo
maadhimisho hayo yatachukua wiki nzima katika eneo la Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.

Wizara, Taasisi na mashirika binafsi wanaotumia nishati ya kuni wametakiwa kuachana na kutumia nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni, Watafiti na taasisi za elimu zatakiwa kufanya utafiti ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Majaliwa amesema kuwa teknolojia hii ya nishati mbadala iendelee kutumika ili watanzania watumie teknolojia mpya ili waondokane na matumizi ya mkaa na kuhamia kwenye teknolojia mpya, Amempongeza mstahiki Meya kwa kuwapa mtaji wajasiriamali ili waweze kubadilisha teknolojia hii mpya.

Vilevile amewashukuru na kuwapongeza wajasiriamali kwa kujitokeza kwa wingi katika kuonyesha ubunifu wao katika kudhibiti na kuokoa mazingira ya nchi,  ambayo itasaidia kusukuma maendeleo ya Taifa.

Pia Waziri Majaliwa amemalizia kwa kusema kuwa siku ambayo ipo kwaajili ya usafi inatakiwa itumike vizuri na kufanya kila siku ni siku ya usafi wa mazingira

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Hamisi Kigwangala, amewataka Wananchi na Taasisi mbalimbali kupunguza matumiza ya mkaa ambayo yamekuwa yakiharibu mazingira na vyanzo vya maji ili kulinda na kuhifadhi na kutunza mazingira.

Vile vile amemhakikishia waziri mkuu wa nchi kuwa mgorogoro ambao uliokuwa unaendelea katika msitu kazimzungwe wameshaumaliza na watazidi kuutunza na kuulinda.



No comments

Powered by Blogger.