Header Ads

Chuo Kikuu Huria wasaini mkataba na mtandao mkubwa


Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), ambayo pia ni mtandao wa radio zenye maudhui ya kijamii nchini. Mtandao huu una radio 31 wanachama zilizopo Tanzania bara na visiwani.

Chini ya mkataba huo, OUT itatumia wataalam wake (wahadhiri) kushiriki katika vipindi mbalimbali vyenye manufaa kwa umma wa watanzania hususan wananchi wanaoishi vijijni, ambapo radio jamii zinafanya shughuli zake. Pia TADIO kupitia radio wanachama, itawajibika kurusha vipindi hivyo kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya.

Mkataba huo unaipa fursa TADIO kuwa na ofisi zake katika majengo ya Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria, Kinondoni Dar es Salaam. Pia unatoa fursa kwa wanafunzi wa OUT wa taaluma ya habari na mawasiliano, kutumia studio zilizopo katika majengo hayo zinazomilikiwa na TADIO kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Pamoja na kutumia studio hiyo, wanafunzi wa OUT watapata pia nafasi ya kushiriki mafunzo kwa vitendo katika radio wananchama zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Bisanda akitoa rai juu ya mkataba huo amesema “OUT itatumia mtandao wa radio wanachama wa TADIO kuifikia jamii na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali za kiuchumi na maendeleo zilizopo kwa kuzingatia vigezo vya utafiti.

No comments

Powered by Blogger.