DC Luoga atofautiana na Madiwani
Na Timothy Itembe, Tarime
Madiwani wa Halmashauri ya Tarime mkoani Mara wametofautiana na Mkuu wa Wilaya, Glorius Luoga kwa kile kinachodaiwa kuwa ameweka mipaka kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi ya wanyamapori TANAPA bila kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika.
Akiongea na mwenyekiti,Yomami Misiwa kutoka chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kwenye baraza la madiwani lililiketi kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleoalisema kuwa madiwani hawatakulaiana na zoezi la mkuu huyo kwenda kuweka mipaka inayotenganisha wananchi wa vijiji hivyo na hifadhi ya Tanapa.
“Sisi kama baraza kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa kanuni ya 26 ya kanuni za kudumu za halmashauri inatupa uhuru wa kujadili na kupitisha jambo lolote bila kuadhiri upande wowote”alisema Misiwa.
Misiwa alitumia nafasi hiyo kuwapa uhuru wa jumbe kupiga kura ya kukataa maamuzi ya mkuu wa wilaya Luoga juu ya kwenda kuweka mipaka inayotenganisha hifadhi na wananchi wa vijiji vinavyozunguka Tanapa ambapo madiwani 15 walipiga kura ya kutaka zoezi hilo kusimama hadi hapo viongozi wa serikali ngazi ya juu watakapo kuja ili kutoa majibu.
Mmoja wa madiwani hao kutoka chama cha Chadema,Mstapha Masyani wa kata ya Kwihancha alisema kuwa zoezi lililoendeshwa na mkuu wa Wilaya Tarime,Glorius Luoga halikushirikisha wananchi wa vijiji husika kwahali hiyo zoezi hilo kuna haja ya kusitishwa.
Naye Lois Manyata Chadema kata ya Kibasuka alisema kuwa Ilani ya Chama cha mapinduzi inadai kuwa zoezi lote la shuguli za maendeleo linalo gusa wananchi lazima wadau washirikishwe ambapo wadau walioshirikishwa ni Tanapa na mkuu huyo hakushirikisha wadau upande wa wananchi kwahali hiyo mchakato wa kuweka mipaka usimame.
Awali mkuu huyo wa wilaya Tarime alitofautiana na Chama chake cha CCM juu ya zoezi hilo ambapo Menyekiti wa ccm wilaya,Daudi Ngicho pamoja na wajumbe wa kamati ya Siasa walichukua hatua ya kutembelea maeneo hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi kuwa mipaka inayowatenganisha na hifadhi imesogezwa kutoka ilipokuwa hapo awali na kuwafuata kwenye makazi yao.
Katibu wa Chama hicho wilaya,Khamis Mukaruka Kura awali alisema kuwa ibara ya 31 ya Chama cha mapinduzi kifungu (a) kinasema kuwa kuendelea kujenga Mahusiano me`ma baina ya mamlaka ya hifadhi za Taifa na Wananchi karibu na hifadhi kwa namna ambayo Wananchi hao watanufaika na uweppo wa hifadhi hiyo.
“Ibara ya 31 kifungu (b) kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi maeneo ya jirani na hifadhi kwa kushirikisha wadau katik akuhakiki mipaka ya maeneo ya maeneo ya hifadhi kwa kuweka alama za kudumu kuandaa mipango ya matumizi bora ya Ardhi na kuzingatia utawala utawala wa sheria katika kusimamia rasilimali za maliasili,” alisema Mukaruka.
Katibu huyo alimaliza kwa kusema kuwa ibara hiyo kifugu (g) kuweka utaratibu wa wazi utakao wawezesha wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kufaidika na maliasili.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya Tarime,Glrius Luoga awali aliwataka madiwani hao kutojadili mchakato mzima wa uliofanyika wa kuweka alama za mipaka huku wakiwataka kusubiri kwani mgogoro huo imefika ngazi ya Taifa na kuwa viongozi watakuja kuutolea majibu.
Aidha Luoga alitumia hisia kali kuwatiisha wajumbe wa baraza la madiwani huku akitumia vijemba katika hotuba yake kwa wanachama wa chama chake cha (CCM).

No comments