Federer anatarajiwa kutangazwa kuwa namba moja dunianii
Mcheza tenisi Roger Federer anatarajiwa kutangazwa kuwa namba moja duniani kwenye viwango vya tenisi kwa wanaume vitakavyotangazwa kesho baada ya kufika fainali ya 'Mercedes Cup'.
Federer raia wa Uswis alitinga fainali hizo zinazofanyika jijini Stuttgart huko Ujerumani kwa kumfunga mpinzani wake katika mchezo wa nusu fainali Nick Kyrgios wa Australia 6-7 (2-7) 6-2 7-6 (7-5).
Mshindi huyo mara 20 a Grand Slam atamng'oa kileleni Rafael Nadal wa Hispania ambaye amedumu kwenye nafasi hiyo kwa takribani wiki moja na siku kadhaa tangu alipotangazwa namba moja baada ya kushinda taji la Wimbledon.
Kwenye fainali itakayoanza saa 8:00 mchana Federer atakabiliana na Milos Raonic wa Canada ambaye amemfunga bingwa mtetezi wa taji hilo Lucas Pouille wa Ufaransa kwa seti (6-4 7-6 (7-3).

No comments