Header Ads

Habari nyingine kubwa kutoka Airtel ni Amsha Amsha


Ni Amsha Amsha! Katika kuonesha inawajali wateja wake, Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kushirikiana na Sportpesa imezindua promosheni mpya ya Amsha Amsha na Airtel Money itakayodumu kwa muda wa mwezi mmoja.

Promosheni hiyo inamtaka mteja wa Airtel Money kuhakikisha anabet siku ambayo droo iko wazi na moja kwa moja na namba yake itaingizwa  kwenye droo ya wiki. Mteja atatakiwa kubet siku ya droo ili kupata nafasi ya kuwa moja ya washindi, amesema.

Isack Nchunda ambaye ni Mkurugenzi  wa Masoko Airtel amesema promosheni hiyo inatoa nafasi nyingine kwa mteja wa Airtel Money kuweza kujishindia zawadi kabambe kwa kubet kwa kutumia Airtel Money.

" Airtel siku zote tunaleta huduma na bidhaa zenye ubunifu na za kutuweka karibu na wateja wetu. Tunaelewa ya kwamba michezo pamoja na mambo ya kubet kwa kutumia Airtel Money, tunaelewa michezo ya kubahatisha imekuwa na maisha ya kawaida kwa wateja wetu, kwa kuzindua promosheni hii ambayo tumeshirikiana na Sportpesa inatoa nafasi nyingine ya kuendelea kutuweka karibu na wateja wetu," amesema Nchuda.

Nchunda amesema droo hiyo itachezeshwa wazi kwa usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania ambayo ndiyo yenye jukumu la kusimamia michezo hiyo nchini. Nchuda ametaja zawadi za kila siku kuwa kuwa ni pamoja na smartphone, jezi za timu za Simba na Yanga pamoja na tiketi za kushuhudia mechi za timu hizo. Zawadi za wiki ni TV yenye nchi 32 pamoja na ving'amuzi vya StarTimes.




No comments

Powered by Blogger.