Kenyatta, naibu wake na watumishi wote wa umma Kukaguliwa Mali Anazomiliki
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa watumishi wote wa umma ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe na naibu wake watafanya ukaguzi wa mali wanazomiliki ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya rushwa nchini Kenya.
Kenyatta alisema katika taarifa hiyo kwamba watumishi wa umma wataulizwa kuelezea chanzo cha utajiri wao na wale wanaopatikana na hatia na uharibifu wa rasilimali za kitaifa watahitajika kueleza chanzo cha utajiri wao.
“Lazima uweze kuelezea jinsi ulivyopata gari lako, nyumba yako na ardhi kwa kulinganisha na kile unachopata,” Kenyatta alisema katika jiji la Mombasa baada ya kuanzisha mradi wa barabara kuu.

No comments