Kubenea aibua ishu ya Makinikia Bungeni
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amemtaka kuwaeleza Dola 190 bilioni zaidi ya Sh424 trilioni zinazopaswa kulipwa na Acacia zitapatikanani lini.
Kubenea ametoa kauli hiyo wakati akichangia bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka 2018/19 leo Juni 1, 2018, Kubenea amesema inasikitisha amesoma kitabu cha bajeti cha waziri na cha kamati hakuna walipozungumzia makinikia.
“Sisi tulitegemea Bunge letu tupewe taarifa ya kina kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na Acacia, tuelezwe Sh424 trilioni ambazo ni Dola bilioni 190 tungepata lakini Bajeti nzima imekuja haijazungumzia na ripoti ya waziri hakuna kokote,” amesema Kubenea.
Pia, kulieleza Bunge majadiliano baina ya Serikali na Kampuni ya Madini ya Acacia kuhusu makinikia yamefikia wapi kwani wananchi wanataka kujua muafaka baina ya kampuni hiyo na serikali.

No comments