Mnyet aitaka Polisi kufanya msako mkali Gogo
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti ameliomba jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wanafuatilia maeneo yote yenye gongo ndani ya mkoa na kuteketeza mitambo inayotumika kutengeneza pombe hiyo.
Mnyeti ametoa agizo hilo wakati akizungumza na jeshi la polisi mkoa wa Manyara katika ziara yake kutembelea Taasisi za kijeshi zilizopo Mjini Babati Manyara ambapo alisema pamoja na jeshi la polisi kufanya vizuri katika kuzuia vitendo vya uhalifu bado wanayo kazi kubwa ya kumaliza Matumizi ya Gongo haswa Dongobesh wilaya ya Mbulu.
Mkuu wa mkoa amesema kinachoharibu mkoa wa Manyara kwa sasa ni upikaji wa pombe haramu aina ya gongo ambayo ana imani kubwa kumalizwa kwa hilo kutachangia wakazi hao kufanya kazi kwa ajili ya kuuendeleza mkoa na taifa kwa jumla.
Alisema'nataka mkakomeshe gongo Dongobesh, ukienda gongo sasa hivi asubuhi muda wa kazi wananchi wote wamelewa, naomba RPC utume kikosi maalum kwa ajili ya kukomesha Gongo Dongobesh, 'alisisitiza Mnyeti.
Mnyeti amesema kuwa zoezi la kuharibu mitambo hiyo lifanywe Wananchi wakisimamiwa na Jeshi la polisi.
Akizungumza kwa niaba ya RPC kamanda Agustino Senga, Kamanda wa kikosi cha usalama bara barani mkoa wa Manyara [RTO] Mary Kipesha alisema wamelipokea agizo la Mkuu wa mkoa na kwamba watalifanyia kazi haraka japo hakusema wanaanza lini zoezi hilo.

No comments