Mo Salah tumaini la Misri dhidi ya Uruguay
Kocha wa timu ya taifa ya Misri Hector Cuper amesema kuna uwezekano wa "karibu 100%" kuwa mshambuliaji Mohamed Salah atacheza mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia mwaka huu leo Ijumaa dhidi ya Uruguay.
Mechi hiyo itachezewa mjini Yekaterinburg na itaanza saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki.
Salah, 25, hajacheza tangu alipoumia begani wakati wa fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mnamo 26 ambapo timu yake ya Liverpool ilishindwa 3-1 na Real Madrid.
"Ninaweza kuwahakikishia karibu 100% kwamba atacheza, pengine kutokee mambo yasiyotarajiwa dakika za mwisho," amesema Cuper.
"Anaweza kuwa mfungaji mabao bora hapa na mmoja wa wachezaji nyota zaidi."
Cuper amesema Salah "anafanya vyema sana" na kwamba alipata nafuu "haraka sana, sana."
Aliongeza: "Tunajaribu kumfanya ajiamini zaidi. Madaktari wanampa fursa ya kuamua kama atacheza au hatacheza, lakini namfahamu Salah vyema sana na nina uhakika kwamba hana wasiwasi, hana woga."
Beki wao Ali Gabr pia anatarajiwa kuwa sawa kucheza baada ya kuumia usoni wakati wa mazoezi.
Uruguay upande wao wanatarajiwa kuchezesha kikosi cha wachezaji wachanga hasa safu ya kati, ambapo watakuwa pia na kiungo wa kati wa miaka 20 Rodrigo Bentancur na Nahitan Nandez, 22.
Lakini kwingineko, kikosi chao kina wachezaji wazoefu, na hata zaidi safu ya mashambulizi ambapo wana Luis Suarez na Edinson Cavani.
Mataifa hayo mawili yamo Kundi A pamoja na Urusi na Saudi Arabia.
Sababu ya wengi kuwapigia upatu Uruguay?
Maandalizi ya mechi hii ya leo jioni yamegubikwa na suala la Mo Salah na iwapo atacheza.
Alijiunga na kikosi cha Misri Jumatano kwa mazoezi ambapo alipasha misuli moto nao, lakini akamaliza sehemu iliyosalia ya mazoezi pekee.
Mechi za leo:

- Misri v Uruguay (saa 9 alasiri Afrika Mashariki)
- Morocco v Iran (saa 12 jioni Afrika Mashariki)
- Ureno v Uhispania (saa 3 usiku Afrika Mashariki)

No comments