Header Ads

Mwanamke ashambuliwa na chatu mpaka kufa


Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa ya hivi karibuni cha mtu kuuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka mmoja.

Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo.

Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu aliye na tumbo limefura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo.

Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani. Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani.

Picha za kutisha zimekuwa zimekisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Indonesiaa zikionysha mwili wa mwakame huyo ukitolewa tumboni mwa chatu huyo mbele ya umati mkubwa.

No comments

Powered by Blogger.