Header Ads

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine


Rais, Dkt. John Magufuli amemteua Prof Andrew Barnabas Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Prof. Pembe umeanza siku ya leo.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Pembe alikuwa Mhadhiri wa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri.




No comments

Powered by Blogger.