RASMI NDAYIRAGIJE KOCHA MPYA KMC
Kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo ya Kinondoni ambayo imedhamiria kufanya vizuri msimu ujao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta ndiye aliyemtambulisha kocha huyo ambapo amesema wameridhishwa na rekodi nzuri ya raia huyo wa Burundi ambaye wanaamini ataisaidia kufika mbali.
Ndayiragije anakumbukwa kwa kuifikisha Mbao fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup msimu wa 2016/17 ambapo walipoteza mbele ya Simba.
"Ni rasmi kuwa Ettiene ndiye kocha mkuu wa KMC kuanzia msimu mpya wa ligi, bodi imeridhishwa na uwezo wake mkubwa na tunaamini atatufikisha mbali," alisema Mstahiki Meya.
Ndayiragije amechukua mikoba ya Fred Minziro ambaye aliipandisha kutoka daraja la kwanza hadi ligi kuu

No comments