Ujerumani chalii, yavunjiwa rekodi na Mexico
Timu ya taifa ya Mexico imekuwa timu ya kwanza kuifunga Ujerumani kwenye mechi yake kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia, katika fainali 7 zilizopita ambapo ilikuwa haijapoteza mchezo.
Bao la winga wa klabu ya PSV ya Uholanzi Hirving Lozano dakika ya 35, limeipa ushindi timu yake ya taifa ya Mexico, dhidi ya Mabingwa watetezi Ujerumani ambao walichukua Kombe hilo nchini Brazil baada ya kuwafunga Argentina bao 1-0.
Katika mechi zake za kwanza Ujerumani imewahi kuzifunga timu za Saudi Arabia mabao 8 mwaka 2002, mabao 4 Costa Rica mwaka 2006, mabao 4 tena Australia mwaka 2010 na mabao 4 Ureno mwaka 2014.
Katika mechi hiyo mlinzi na nahodha wa Mexico Rafael Márquez aliyeingia kipindi cha pili amefikia rekodi ya mchezaji wa zamani wa Mexico Antonio Carbajal na Lothar Matthäus wa Ujerumani ya kucheza Fainali 5 tofauti za Kombe la Dunia.

No comments