Header Ads

Uporaji wa fedha waongezeka Afrika Kusini


Takriban kila siku nchini Afrika Kusini, kampuni za kusafirisha hela hulengwa na majambazi wanaowavamia na kuwapora. Hata baadhi ya matukio huhusisha utumiaji wa vilipuzi.

Mamilioni ya fedha hutoweka kila siku chini ya mikononi mwa majambazi sugu baadhi yao wakiwa gerezani. Aidha, Maafisa wa polisi wametajwa kuhusika katika baadhi ya wizi.

Kumekuwa na visa 378 vya uporaji wa pesa ikimaanisha ongezeko la asilimia 104% kati ya mwaka 2016 na 2017.

Huenda hali ikawa mbaya zaidi mwaka huu kwani, kati ya mwezi Mei mwaka uliopita hadi Januari mwaka huu pekee, visa 153 vya uporaji vimeripotiwa ikiwa ni zaidi ya tukio moja kila siku.

Usafirishajii wa pesa kutumia magari yasiyopenya risasi haujaboresha hali kwani wezi hao huyalipua magurudumu kabla ya kutumia vilipuzi kufungua milango ya magari yanayosafirisha pesa.

Baadhi ya walinzi hulengwa pindi wanapotoka wakibeba pesa kutoka ofisi zao wakielekea kuziingisha kwenye gari.

Anneliese Burgess, ni mwandishi wa habari ambaye ametumia miaka ya hivi karibuni kufanya uchunguzi kwa minajili ya kitabu chake, 'Heist! South Africa's cash-in-transit epidemic'.

"Visa hivi vinashtua kabisa: Wanawavamia watu, na kuwatupia risasi," Anneliese ameiambia BBC.

No comments

Powered by Blogger.