Wachimbaji wadogo wa dhahabu kuanza kuneemeka
Serikali imeanza kuchukua hatua madhubuti ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Shinyanga kwa kuweka miundombinu sahihi ya uchimbaji na kujenga kiwanda cha kuchenjulia dhahabu lengo likiwa ni kuwawezesha watanzania kunufaika na sekta ya Madini na kupunguza gharama za uzalishaji.
Akizungumza na baadhi ya wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu baada ya kutembelea na kukagua kiwanda kidogo cha kuchenjulia dhahabu kinachojengwa mjini Shinyanga Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema serikali imeanza kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo na kuzitatua.
Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wameiomba serikali kuendelea kufanyia kazi kero zinazowakwamisha katika shughuli zao za uchimbaji huku baadhi ya wadau wa sekta ya Madini wakiiomba serikali kutoyumbishwa na baadhi ya watu wachache wanaotanguliza maslahi binafsi mbele kwa lengo la kujinufaisha wenyewe.
Kwa upande wake kamishna msaidizi wa Madini kanda ya kati na Magharibi Joseph Kumburu amesema kero zinazolalamikiwa na wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu zimeshaanza kufanyiwa kazi katika ngazi ya kanda.

No comments