Header Ads

Mchekeshaji BwanaMjeshi amchana Manara laivu “Aache maneno ya kwenye Kanga tukutane kwenye Ligi”

Mchekeshaji kutoka katika kundi la Timamu BwanaMjeshi amefunguka kuhusu kazi zake pamoja pamoja na kazi wanazotarajia kuziachia kwa ajili ya kujitengenezea mazingira mazuri ya kikazi.
BwanaMjeshi ameogea hayo wakati anapiga stori na BongoFive na kusema kuwa “kufanya kwangu vizuri ni kwa kuwa najua kuishi na watu vizuri hata mwanamke anayedumu kwenye familia ni yule anaishi vizuri na mume wake ndo mana nimeweza kufanya kazi na kila mtu bila tatizo lolote”
Lakini pia BwanaMjeshi amefunguka kuhusu ukaribu wake na Mkaliwenu na kusema kuwa wao ni washikaji ila sio kihivyo bali huwa nasalimiana naye tukionana ila sio ushikaji wa kwenye simu”
Mbali na kuongelea hayo pia amefunguka kuhusu dhumuni la kutunga wimbo unaihusu klabu ya Yanga na kusema kuwa:- ” Kilichonifanya nitunge wimbo huo ni kwa kuwa mini shabiki wa Yanga na mkereketwa wa klabu hii lakini pia hisia ndo zilinifanya niimbe wimbo kama huu kwani watu wanaikejeli sana klabu yangu kwa kuwa eti imekuwa na matokeo mabaya wanashindwa kuelewa kuwa  haya ni mapito tu”
BwanaMjeshi aliongeza ” kingine kilichonifanya nitoe wimbo huu ni Msemaji wa Simba Haji Manara mana yule jamaa anaongea sana,aachane na maneno ya kwenye kanga mana jamaa anatwiti vitu vya ajabu ajabu anashindwa kuwaachia maneno haya mapaparazi,Manara acha maneno tukutane uwanjani mana tuko kwenye chimbo la maana tukirudi itakuwa balaa”
Klabu ya Yanga jana imeshinda mchezo wake wa kwanza katika Mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu kutoka nchini Algeria inayoitwa USM Algers.

By Ally Juma


No comments

Powered by Blogger.