Header Ads

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MAGUMBA ATEMBELEA TPA

 Naibu Meneja wa Bandari  Utekelezaji, Ahmed Mchalaganya, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi TPA inavyohudumia shehena ya mizigo inayopita bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba akitoa maelekezo kwa maofisa wa kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho bandarini. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
 Afisa Mkaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo bandarini, Bw. Deogratias Mosha, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo kinavyofanya kazi zake bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo,  Omary Mgumba akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na baadae kufanya ziara bandarini kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. 


No comments

Powered by Blogger.