Header Ads

TRC YAAHIDI KUSAIDIA MAENDELEO YA ELIMU WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jockate Mwegelo (wa nne kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (wa tatu kulia), wafanyakazi wa Wilaya ya Kisarawe, TRC pamoja na wawakilishi kutoka Mkandarasi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR Yapi Merkezi wakijadili namna ambavyo wanaweza kusaidia maendeleo ya Elimu wilayani Kisarawe katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Septemba 22. 2018. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) kwa niaba ya TRC akimuahidi mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (kushoto) kujenga Madarasa na kuchangia Vyakula ikiwemo Maharage, Mchele na Mafuta ya kupikia kwa wanafunzi walio kambini wakati wa Harambee ya kuchangia maendeleo ya Elimu katika Kampeni ya 'Tokomeza Ziro' iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Septemba 22, 2018.
 Picha ya pamoja baada ya mazungumzo


No comments

Powered by Blogger.