Sudan yatuma wanajeshi zaidi mpakani na Ethiopia Vikosi vya jeshi la Sudan
vimetuma wanajeshi zaidi kwenye mpaka unaozozaniwa na Ethiopia, na kutangaza kuwa wana udhibiti kamili wa eneo hilo huku kukiwa na mvutano na Addis Ababa.
Jeshi lilituma ujumbe wa kuwatuliza wananchi, na kuwaambia "walale fofofo". Sudan ilitangaza tarehe 1 Disemba kwamba wanajeshi wake walikuwa wamesambaratisha makaazi ya Waethiopia na kuyadhibiti baada ya kurushiana risasi na vikosi vya nchi hiyo jirani katika eneo la al-Fashaga.
Ilifuatia ripoti kwamba wanajeshi 21 wa Sudan waliuawa na wengine 30 kujeruhiwa katika mapigano na wanajeshi wa Ethiopia katika eneo la Birkat Nourain huko al-Fashaga tarehe 27 Novemba.
Mapigano hayo mapya yalimfanya mtawala wa kijeshi wa Sudan, Luteni Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, kuapa kwamba nchi yake "haitaachia inchi moja" ya eneo lake kwa Ethiopia.
No comments