Atletico Madrid kuishtaki Barcelona, Fifa
Inadaiwa kuwa wiki iliyopita Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu aikutana na baadhi ya watu wa familia ya Griezmann kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumnasa mchezaji huyo.
Griezmann alisaini mkataba mpya na Atletico Madrid msimu uliopita ambao utafika kikomo mwaka 2021.
Kwa mujibu wa sheria za Fifa zinasema endapo timu ikiwa inataka kumsajili mchezaji lazima iwasiliane na klabu yake anayoichezea kabla ya kuruhusiwa kufanya mazungumzo. Endapo FIFA itabaini kuwa Barca wamefanya kosa hilo wanaweza kufungiwa kufanya usajili katika kipindi cha msimu mmoja mpaka miwili.
No comments