Mkuregenzi wa fedha NHC mrithi Mchechu

Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Felix Maagi ameteuliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Nehemia
Mchechu aliyesimamishwa kupisha uchunguzi.
Mchechu alisimamishwa kazi Desemba 16,2017 na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kupisha uchunguzi
wa tuhuma dhidi yake ambazo hazijawekwa wazi wala mamlaka inayochunguza.
Akizungumza jana Jumanne Desemba 19,2017 kuhusu
mikakati yake baada ya kuteuliwa na Bodi ya NHC kukaimu nafasi hiyo
Maagi alisema, ‘’Kwa sasa siwezi kusema kitu kwa kuwa hata ofisi bado
sijakabidhiwa.”
“Nikikabidhiwa na nikiingia ofisini nitakuwa na cha kuzungumza lakini kwa sasa sina cha kusema,” alisema.
Maagi ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika usimamizi
wa biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha Esami nchini Uganda na ni mhasibu
anayetambulika na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
(NBAA).
No comments