JAFO AKERWA NA UCHAFU SOKO LA MABIBO.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani jafo akifanya ukaguzi katika soko la mabibo.
Wafanyabiashara wa soko la mabibo wakitoa malalamiko yao kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo.
............................................................................
WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na
uchafu uliokithiri katika soko la Mabibo lililopo wilayani Ubungo
jijini Dar as salaam.
Soko hilo maarufu kwa jina la Mabibo-mahakama ya ndizi limetapakaa maji machafu na madibwi yanayotoa harufu mbaya.
Jafo amesema
uchafu huo ni hatari sana kwa afya ya wananchi kwani wanaweza kupata
magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Kutokana na
hali hiyo, Jafo ameielekeza manispaa ya ubungo kufanya marekebisho ya
haraka ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi na kusambaza kokoto sokoni
hapo pamoja na kuweka mfereji wa kupitishia maji.
Pia Jafo amewataka watendaji wa soko hilo kusimamia mapato ipasavyo kutokana na ukusanyaji mapato kuwa hauridhishi.
Amesema
wastani wa sh.milioni 90 kwa mwezi zinakusanywa ikilinganishwa na
biashara kubwa ya ndizi na viazi inayofanywa sokoni hapo.



No comments