Jeshi la polisi lapiga marufuku upigaji fataki
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limepiga marufuku kufyatua fataki siku ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya.
Baada ya katazo hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kukusanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe ndipo wataruhusiwa kufyatua milipuko hiyo.
“Mwananchi yeyote haruhusiwi kupiga fataki eneo lolote isipokuwa kwenye viwanja hivyo wanapotakiwa kukusanyika na kupiga milipuko hiyo kwa nusu saa tu ambapo ulinzi utaimarika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika eneo hilo,’’ alisema Kamanda Mambosasa.
Aidha Kamanda Mambosasa alisema upigaji wa fataki hizo umekuwa ukifanyika kiholela na kusababisha baadhi ya wananchi kupata mshtuko unaosababisha ugonjwa wa moyo
Hata hivyo alieleza kuwa jeshi hilo limebaini siku ya mkesha wanapofyatua fataki hizo baadhi yao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu na kupora mali mbalimbali za wananchi.
No comments