Jux atumia ujumbe huu vanessa mdee baada kusaini univursal music group
Ni raha kuona mtu wako wa karibu anafanikiwa kupiga
hatua kwenye jambo fulani. Jux ameonyesha kufurahia mafanikio ambayo
anayapata mpenzi wake Vanessa Mdee.
Baada ya mrembo huyo wa Bounce kusaini dili nono na
kampuni ya Universal Music Group, Jux ameonyesha kushindwa kuzuia hisia
zake kwa kumpongeza Vee Money kupitia mtandao wa Instagram.
Kupitia mtandao huo Jux ameandika:
@universalmusicgroup @universalmusicgermany Najua
unandoto kubwa sana kufika unapotaka na kila siku nakwambia inawezekana
utafika tu hii ni moja ya njia kuelekea uko. hongera mama @vanessamdee
you deserve this. Safari inaendelea #moneymondays #independentwoman
#powerful #africanqueen #smart #cashmadame💰 #levels

No comments