Header Ads

Waziri Makamba azindua kamati ya ushauri wa mazingira


Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba imezindua kamati ya Taifa ya ushauri wa mazingira ambayo itakuwa ikijihusisha na uchunguzi wa masuala yanayohusu kulinda mazingira.

Akizungumza jna waandishi wa habari jana Mjini Dodoma, Makamba alisema kuwa Kamati ya mazingira itaundwa na wajumbe wenye uzoefu katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa mazingira.
‘Kifungu namna 11 cha sheria ya mazingira kinasema itaanzishwa kamati ya Taifa ya ushauri wa mazingira itakayo mshauri Waziri kifungu namna 11;1 cha sheria kinasema itanzishwa Kamati ya taifa ya ushauri wa Mzingira itakayo mshauri waziri katika haya mamlaka ambayo nimeyazungumza,’alisema Makamba.
‘Kamati ya mazingira itaundwa na wajumbe wenye uzoefu katika maeneo mbalimbali ya usimamizi wa mazingira kwenye sekta ya umma binafsi na vyama vya kiraia na kwamba iwe ni ya kitaalam.’
Katibu mkuu wa wizara hiyo, Joseph Malongo alisema kamati hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria na kwamba wananchi wanapaswa kujua na kuzingatia umuhimu wa mazingira katika kila jambo.

No comments

Powered by Blogger.