Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa
Mwanamke Asha Jeremiah (32), amekamatwa kwa kosa la kukutwa na gunia la
bangi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda Msangi amesema Jeshi hilo linaendelea na upepelezi pamoja na
msako katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Wilayani Ukerewe na pindi
upelelezi utakapokamilika Asha atafikishwa mahakamani.
Asha mkazi wa Kisiwa cha Lyegoba, anashikiliwa kwa kosa la kupatikana na
bangi ikiwa kwenye gunia moja lililojaa, maboksi matatu yaliyojaa
bhangi na misokoto ya bhangi 371, vyote vikikadiriwa kuwa na uzito wa
kilogramu kati ya 35 hadi 50, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Msangi ameeleza kuwa askari walipokea taarifa kutoka kwa raia wema juu
ya uwepo wa mtu anayejihusisha na uuzaji wa bangi katika Kisiwa cha
Lyegoba na baada ya ufuatiliaji ndipo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa
akiwa na bangi hiyo.
Aidha, Msangi ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza kuacha
kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha sheria na kuendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufanikisha kukamatwa kwa waharifu.
No comments