NABII Josephat Mwingira amedai mahakamani kwamba hayuko tayari kupima
kipimo cha DNA na hawezi kulipa fidia ya Sh bilioni saba kwa sababu
hajawahi kuzaa wala kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Dk. William
Morris.
Nabii Mwingira alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini alipokuwa akijitetea kuhusu madai
dhidi yake kwamba alizini na kuzaa na Dk. Philis Nyimbi ambaye ni mke wa
Dk. Morris.
“Sifanyi vitu ambavyo sihusiki, aliyebeba mimba ndiye anajua mtoto wa
nani, amuulize mkewe mtoto kazaa na nani, uchungaji wangu ni wa Mungu,
siwezi kusafishwa kwa DNA,” alidai.
Mahojiano ya Nabii Mwingira na Wakili Peter Swai aliyekuwa akimuongoza kutoa utetezi wake yalikuwa kama ifuatavyo:
Swali: Tuambie cheo chako ni nani?
Jibu: Cheo cha kiroho ni Nabii na Mtume.
Swali: Unafanya mahuburi wapi?
Jibu: Efatha.
Swali: Unamfahamu Dk. Philis na Dk. Morris?
Jibu: Nawahafamu wote, ni mtu na muewe, walikuwa washiriki wa kituoni
kwangu Efatha, Dk. Nyimbi ni mtoto wa nyumbani, nilisoma na kaka zake,
majirani kijijini kwetu.
Swali: Mnatokea kijiji gani?
Jibu: Tunatokea Kijiji cha Mbaha wilayani Nyasa.
Swali: Kuna siku ambayo Dk. Morris alikuwa na ombi lolote kwako?
Jibu: Walikuja na mkewe kuomba msaada wa fedha kwa ajili ya kununua vitu katika mnada bandarini?
Swali: Shilingi ngapi?
Jibu: Ni zaidi ya Sh milioni 16, niliwapa kutoka katika akaunti ya Efatha, lakini mpaka leo hawajarudisha.
Swali: Hivyo vitu uliviona?
Jibu: Niliviona, ni kama vile vitu vinavyookotwa Marekani, nilishangaa anasafirisha takataka kutoka Marekani mpaka huku.
Swali: Ulishawahi kufuatwa na Morris kukulalamikia kwamba una mahusiano ya kimapenzi na mkewe?
Jibu: Ha ha ha ha, hapana.
Swali: Unafahamu kwamba Dk. Nyimbi ana mtoto?
Jibu: Nafahamu.
Swali: Kuna siku hata moja aliwahi kukwambia baba wa huyo mtoto?
Jibu: Hapana hatujawahi kuongelea kitu kama hicho.
Swali: Ulishawahi kuhusishwa katika mgogoro wa mtoto wa Dk. Nyimbi?
Jibu: Kwani Morris anasema mtoto sio wake?
Swali: Kuna tuhuma hapa, Morris anadai yule mtoto umezaa na Dk. Nyimbi.
Jibu: Niliwahi kusoma katika magazeti, sijawahi kuletewa mtoto, lakini nikiletewa nitalea.
Swali: Inasemekena wewe ulishiriki katika kikao cha familia kilichotambua mtoto ni wako.
Jibu: Hapana.
Swali: Kuna madai hapa mahakamani, Morris anaomba umlipe fidia ya Sh bilioni saba kwa kuwa na mahusiano na mkewe, unasemaje?
Jibu: Tunaanzaje? Unapolipa lazima uwe umetumia kile kitu, hilo jambo halipo.
Swali: Unazungumziaje madai yaliyopo mahakamani?
Jibu: Kama hii mahakama inatenda haki, itaangalia kwa haki, Dk Morris atalipa gharama za kunisumbua.
Swai alimaliza kumwongoza mteja wake na mahakama ikatoa nafasi kwa Wakili wa mlalamikaji, Respicius Ishengoma kumuhoji maswali.
Swali: Naomba nikuite Mchungaji?
Jibu: Umetoa wapi hilo jina?
Swali: Nini tofauti ya Mchungaji na Nabii?
Jibu: Mchungaji na Nabii ni tofauti sana, kama ukisema hakimu na wakili, huoni tofauti? Kila mmoja ana kazi yake.
Swali: Ndiyo maana nimekuuliza kutaka kujua tofauti.
Jibu: Mimi nahubiri injili, sifanyi kazi moja tu ya kuchunga, ila nina wachungaji chini yangu.
Swali: Una watoto wangapi?
Jibu: Nina watoto sita, lakini mmoja marehemu.
Swali: Wataja majina.
Jibu: Lucy, Joshua, Anna, Jonath na Glory.
Swali: Glory alizaliwa lini?
Jibu: Alizaliwa 2007.
Swali: Nikisema kazaliwa Mei 22 mwaka 2007 utakubaliana na mimi?
No comments