Mgombea ubunge jimbo la Nyalandu abadili gia angani

SIKU moja baada ya NEC kuanika majina
ya wagombe huku jina lake likitajwa kuwa miongoni mwao, Djumbe Joseph
aliyepitishwa na (NEC) kugombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kwa
tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameandika barua
ya kujitoa katika uchaguzi mdogo ambao unatarajiwa kufanyika Januari 13,
2018 kwa kile alichosema anafuata msimamo wa chama chake.
Akizungumza na waandishi wa habari
Djumbe amesema kuwa ameamua kuungana na viongozi wakuu wa chama chake
kutoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ambao unategemewa kufanyika mapema
Januari 2018.
Chadema jana kilitangaza kuwa hakiweka
muakilishi yoyote kugombea jimbo hilo la Singida Kaskazini kwa kile
walichosema awali kuwa hawawezi kushiriki uchaguzi huo wa marudio bila
tathimini kufanyika juu ya uchaguzi wa udiwani uliofanyika hivi karibuni
ambao walidai ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki na sheria.
No comments