MUIGIZAJI mwenye kiwango kizuri kwenye tasinia ya filamu Bongo, Jennifer
Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa ayumbishwi na ndoa wanazofunga baadhi ya
mastaa hivi karibuni kwani wakati wake ukifika na
yake itafanyika.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Odama alisema kuwa hakuna kitu kizuri
duniani kama wakati wa Mungu ambao ndio sahihi, hivyo hawezi kuona mtu
amefanya kitu na yeye akatamani
kwasababu mwingine amefanya.
“Mimi naamini kabisa kila jambo lina wakati wake na wakati mzuri ni
Mungu aliokupangia jambo husika, sio tu kukurupuka kwasababu mwingine
kafanya,” alisema Odama
No comments